Native Bible

1 Kings 3:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Wakati wa usiku mwana wa huyu mwanamke akafa kwa sababu alimlalia.

1 Kings 3:19 in English

1 Kings 3:19 · Berean Standard Bible

During the night this woman’s son died because she rolled over on him.

Context

17Mmojawapo akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami. 18Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba isipokuwa sisi wawili. 19“Wakati wa usiku mwana wa huyu mwanamke akafa kwa sababu alimlalia. 20Hivyo akaondoka katikati ya usiku na kumchukua mwanangu kutoka ubavuni pangu wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa nimelala. Akamweka kifuani mwake na kumweka mwanawe aliyekufa kifuani mwangu. 21Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia sana katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyekuwa nimemzaa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.