1 Wafalme 2:10
1 Kings 2:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Daudi akapumzika pamoja na baba zake naye akazikwa katika Mji wa Daudi.
1 Kings 2:10 in English
1 Kings 2:10 · Berean Standard Bible
Then David rested with his fathers and was buried in the City of David.
Context
8“Ukumbuke, unaye Shimei mwana wa Gera, Mbenyamini kutoka Bahurimu, ambaye alinilaani kwa laana kali siku niliyokwenda Mahanaimu. Aliposhuka kunilaki huko Yordani, nilimwapia kwa Bwana: ‘Sitakuua kwa upanga!’ 9Lakini sasa, usidhani kwamba hana hatia. Wewe ni mtu wa hekima, utajua la kumtendea. Zishushe mvi zake kaburini kwa damu.” 10Kisha Daudi akapumzika pamoja na baba zake naye akazikwa katika Mji wa Daudi. 11Daudi alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu. 12Kwa hiyo Solomoni akaketi katika kiti cha ufalme cha baba yake Daudi, nao utawala wake ukaimarika sana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.