1 Wafalme 2:11
1 Kings 2:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
1 Kings 2:11 in English
1 Kings 2:11 · Berean Standard Bible
The length of David’s reign over Israel was forty years—seven years in Hebron and thirty-three years in Jerusalem.
Context
9Lakini sasa, usidhani kwamba hana hatia. Wewe ni mtu wa hekima, utajua la kumtendea. Zishushe mvi zake kaburini kwa damu.” 10Kisha Daudi akapumzika pamoja na baba zake naye akazikwa katika Mji wa Daudi. 11Daudi alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu. 12Kwa hiyo Solomoni akaketi katika kiti cha ufalme cha baba yake Daudi, nao utawala wake ukaimarika sana. 13Basi Adoniya, mwana wa Hagithi, akaenda kwa Bathsheba, mama yake Solomoni. Bathsheba akamuuliza, “Je, umekuja kwa amani?”
Akajibu, “Ndiyo, kwa amani.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.