Native Bible

1 Corinthians 7:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa.

1 Corinthians 7:9 in English

1 Corinthians 7:9 · Berean Standard Bible

But if they cannot control themselves, let them marry. For it is better to marry than to burn with passion.

Context

7Laiti watu wangekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa kipawa chake kutoka kwa Mungu, mmoja ana kipawa cha namna hii na mwingine ana cha namna ile. 8Kwa wale wasiooa na kwa wajane, nasema hivi, ingekuwa vizuri wasioe. 9Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa. 10Kwa wale waliooana nawapa amri (si mimi ila ni Bwana): Mke asitengane na mumewe. 11Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.