1 Wakorintho 12:21
1 Corinthians 12:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na ninyi!”
1 Corinthians 12:21 in English
1 Corinthians 12:21 · Berean Standard Bible
The eye cannot say to the hand, “I do not need you.” Nor can the head say to the feet, “I do not need you.”
Context
19Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20Kama ulivyo, una viungo vingi, lakini mwili ni mmoja. 21Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na ninyi!” 22Lakini badala yake, vile viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa dhaifu, ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana. 23Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.