1 Wakorintho 10:15
1 Corinthians 10:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nasema watu wenye ufahamu, amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo.
1 Corinthians 10:15 in English
1 Corinthians 10:15 · Berean Standard Bible
I speak to reasonable people; judge for yourselves what I say.
Context
13Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili. 14Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu. 15Nasema watu wenye ufahamu, amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. 16Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.