1 Nyakati 7:23
1 Chronicles 7:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake.
1 Chronicles 7:23 in English
1 Chronicles 7:23 · Berean Standard Bible
And again he slept with his wife, and she conceived and gave birth to a son. So he named him Beriah,* because tragedy had come upon his house.
Context
21Tahathi akamzaa Zabadi,
na Zabadi akamzaa Shuthela.
Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. 22Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. 23Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. 24Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera. 25Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu,
Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.