Native Bible

1 Chronicles 7:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji.

1 Chronicles 7:22 in English

1 Chronicles 7:22 · Berean Standard Bible

Their father Ephraim mourned for many days, and his relatives came to comfort him.

Context

20Wana wa Efraimu walikuwa: Shuthela, ambaye alimzaa Beredi, Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada, Eleada akamzaa Tahathi, 21Tahathi akamzaa Zabadi, na Zabadi akamzaa Shuthela. Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. 22Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. 23Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. 24Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.