1 Nyakati 7:21
1 Chronicles 7:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tahathi akamzaa Zabadi, na Zabadi akamzaa Shuthela. Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao.
1 Chronicles 7:21 in English
1 Chronicles 7:21 · Berean Standard Bible
Zabad his son, and Shuthelah his son. Ezer and Elead were killed by the natives of Gath, because they went down to steal their livestock.
Context
19Wana wa Shemida walikuwa:
Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu. 20Wana wa Efraimu walikuwa:
Shuthela, ambaye alimzaa Beredi,
Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada,
Eleada akamzaa Tahathi, 21Tahathi akamzaa Zabadi,
na Zabadi akamzaa Shuthela.
Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. 22Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. 23Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.