1 Nyakati 6:49
1 Chronicles 6:49 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu.
1 Chronicles 6:49 in English
1 Chronicles 6:49 · Berean Standard Bible
But Aaron and his sons did all the work of the Most Holy Place.* They presented the offerings on the altar of burnt offering and on the altar of incense to make atonement for Israel, according to all that Moses the servant of God had commanded.
Context
47mwana wa Mahli,
mwana wa Mushi, mwana wa Merari,
mwana wa Lawi. 48Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu. 49Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu. 50Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni:
Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua, 51Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.