1 Nyakati 27:23
1 Chronicles 27:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani.
1 Chronicles 27:23 in English
1 Chronicles 27:23 · Berean Standard Bible
David did not count the men aged twenty or under, because the LORD had said that He would make Israel as numerous as the stars of the sky.
Context
21kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;
kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri; 22kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.
Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli. 23Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. 24Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi. 25Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme.
Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.