1 Nyakati 27:22
1 Chronicles 27:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu. Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli.
1 Chronicles 27:22 in English
1 Chronicles 27:22 · Berean Standard Bible
and over Dan was Azarel son of Jeroham. These were the leaders of the tribes of Israel.
Context
20kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia;
kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya; 21kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;
kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri; 22kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.
Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli. 23Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. 24Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.