1 Nyakati 26:15
1 Chronicles 26:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe.
1 Chronicles 26:15 in English
1 Chronicles 26:15 · Berean Standard Bible
The lot for the South Gate fell to Obed-edom, and the lot for the storehouses to his sons.
Context
13Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo. 14Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia.* Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 15Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 16Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.
Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: 17Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.