Native Bible

1 Chronicles 26:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.

1 Chronicles 26:13 in English

1 Chronicles 26:13 · Berean Standard Bible

They cast lots for each gate, according to their families, young and old alike.

Context

11Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu. 12Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 13Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo. 14Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia.* Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 15Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.