1 Nyakati 26:12
1 Chronicles 26:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo.
1 Chronicles 26:12 in English
1 Chronicles 26:12 · Berean Standard Bible
These divisions of the gatekeepers, through their chief men, had duties for ministering in the house of the LORD, just as their brothers did.
Context
10Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza), 11Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu. 12Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 13Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo. 14Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia.* Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.