1 Nyakati 22:14
1 Chronicles 22:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,000* za dhahabu, talanta 1,000,000* za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza.
1 Chronicles 22:14 in English
1 Chronicles 22:14 · Berean Standard Bible
Now behold, I have taken great pains to provide for the house of the LORD—100,000 talents of gold,* 1,000,000 talents of silver,* and bronze and iron too great to be weighed. I have also provided timber and stone, and you may add to them.
Context
12Bwana na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya Bwana Mungu wako. 13Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria Bwana alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa. 14“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,000* za dhahabu, talanta 1,000,000* za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. 15Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi 16wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.