Native Bible

1 Chronicles 22:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.”

1 Chronicles 22:16 in English

1 Chronicles 22:16 · Berean Standard Bible

in gold and silver, bronze and iron—craftsmen beyond number. Now begin the work, and may the LORD be with you.”

Context

14“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,000* za dhahabu, talanta 1,000,000* za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. 15Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi 16wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.” 17Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe. 18Akawaambia, “Je, Bwana Mungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini ya Bwana na watu wake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.