1 Nyakati 22:15
1 Chronicles 22:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi
1 Chronicles 22:15 in English
1 Chronicles 22:15 · Berean Standard Bible
You also have many workers: stonecutters, masons, carpenters, and men skilled in every kind of work—
Context
13Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria Bwana alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa. 14“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,000* za dhahabu, talanta 1,000,000* za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. 15Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi 16wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.” 17Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.