Native Bible

1 Chronicles 17:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.

1 Chronicles 17:15 in English

1 Chronicles 17:15 · Berean Standard Bible

So Nathan relayed to David all the words of this entire vision.

Context

13Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia. 14Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ” 15Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya. 16Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema: “Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? 17Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, Ee Bwana Mungu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.