1 Nyakati 17:14
1 Chronicles 17:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ”
1 Chronicles 17:14 in English
1 Chronicles 17:14 · Berean Standard Bible
But I will set him over My house and My kingdom forever, and his throne will be established forever.”
Context
12Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele. 13Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia. 14Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ” 15Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya. 16Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema:
“Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.