Native Bible

1 Chronicles 16:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana:

1 Chronicles 16:7 in English

1 Chronicles 16:7 · Berean Standard Bible

On that day David first committed to Asaph and his brothers this song of thanksgiving to the LORD:

Context

5Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, 6nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu. 7Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana: 8Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. 9Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa; waambieni matendo yake yote ya ajabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.