Sefania 3:10
Zephaniah 3:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kutoka ngʼambo ya mito ya Kushi watu wangu wanaoniabudu, watu wangu waliotawanyika, wataniletea sadaka.
Zephaniah 3:10 in English
Zephaniah 3:10 · Berean Standard Bible
From beyond the rivers of Cush * My worshipers, My scattered people, will bring Me an offering.
Context
8Bwana anasema,
“Kwa hiyo ningojee mimi,
siku nitakayosimama kuteka nyara.
Nimeamua kukusanya mataifa,
kukusanya falme
na kumimina ghadhabu yangu juu yao,
hasira yangu kali yote.
Dunia yote itateketezwa
kwa moto wa wivu wa hasira yangu. 9“Ndipo nitatakasa midomo ya mataifa,
kwamba wote waweze kuliitia jina la Bwana
na kumtumikia kwa pamoja. 10Kutoka ngʼambo ya mito ya Kushi
watu wangu wanaoniabudu,
watu wangu waliotawanyika,
wataniletea sadaka. 11Siku hiyo hutaaibishwa
kwa ajili ya makosa yote ulionitendea,
kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huu
wale wote wanaoshangilia
katika kiburi chao.
Kamwe hutajivuna tena
katika kilima changu kitakatifu. 12Lakini nitakuachia ndani yako
wapole na wanyenyekevu,
ambao wanatumaini jina la Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.