Zekaria 6:4
Zechariah 6:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”
Zechariah 6:4 in English
Zechariah 6:4 · Berean Standard Bible
So I inquired of the angel who was speaking with me, “What are these, my lord?”
Context
2Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, 3la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. 4Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?” 5Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. 6Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.