Native Bible

Zechariah 12:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu.

Zechariah 12:9 in English

Zechariah 12:9 · Berean Standard Bible

So on that day I will set out to destroy all the nations that come against Jerusalem.

Context

7“Bwana atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda. 8Katika siku hiyo, Bwana atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa Bwana akiwatangulia. 9Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu. 10“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema* na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. 11Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.