Native Bible

Zechariah 12:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema* na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.

Zechariah 12:10 in English

Zechariah 12:10 · Berean Standard Bible

Then I will pour out on the house of David and on the people of Jerusalem a spirit * of grace and prayer, and they will look on Me,* the One they have pierced.* They will mourn for Him as one mourns for an only child, and grieve bitterly for Him as one grieves for a firstborn son.

Context

8Katika siku hiyo, Bwana atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa Bwana akiwatangulia. 9Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu. 10“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema* na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. 11Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido. 12Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.