Native Bible

Zechariah 11:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Bwana akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu.

Zechariah 11:15 in English

Zechariah 11:15 · Berean Standard Bible

And the LORD said to me: “Take up once more the equipment of a foolish shepherd.

Context

13Naye Bwana akaniambia, “Mtupie mfinyanzi,” hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba ya Bwana. 14Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli! 15Kisha Bwana akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. 16Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao. 17“Ole wa mchungaji asiyefaa, anayeliacha kundi! Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume! Mkono wake na unyauke kabisa, jicho lake la kuume lipofuke kabisa!”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.