Wimbo 8:12
Song of Songs 8:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini shamba langu la mizabibu ambalo ni langu mwenyewe ni langu kutoa; hizo shekeli 1,000 ni kwa ajili yako, ee Solomoni, na shekeli mia mbili* ni kwa ajili ya wale wanaotunza matunda yake.
Song of Songs 8:12 in English
Song of Songs 8:12 · Berean Standard Bible
But my own vineyard is mine to give; the thousand shekels are for you, O Solomon, and two hundred are for those who tend its fruit.
Context
10Mimi ni ukuta,
nayo matiti yangu ni kama minara.
Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake
kama yule anayeleta utoshelevu. 11Solomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni;
alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji.
Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake
shekeli 1,000* za fedha. 12Lakini shamba langu la mizabibu
ambalo ni langu mwenyewe
ni langu kutoa;
hizo shekeli 1,000 ni kwa ajili yako, ee Solomoni,
na shekeli mia mbili* ni kwa ajili
ya wale wanaotunza matunda yake. 13Wewe ukaaye bustanini
pamoja na marafiki mliohudhuria,
hebu nisikie sauti yako! 14Njoo, mpenzi wangu,
uwe kama swala
au kama ayala kijana
juu ya milima iliyojaa vikolezo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.