Wimbo 7:3
Song of Songs 7:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Matiti yako ni kama wana-paa wawili, mapacha wa paa.
Song of Songs 7:3 in English
Song of Songs 7:3 · Berean Standard Bible
Your breasts are like two fawns, twins of a gazelle.
Context
1Ee binti wa mwana wa mfalme,
tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu!
Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani,
kazi ya mikono ya fundi stadi. 2Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo
ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa.
Kiuno chako ni kichuguu cha ngano
kilichozungukwa kwa yungiyungi. 3Matiti yako ni kama wana-paa wawili,
mapacha wa paa. 4Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu.
Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni
karibu na lango la Beth-Rabi.
Pua lako ni kama mnara wa Lebanoni
ukitazama kuelekea Dameski. 5Kichwa chako kinakuvika taji kama mlima Karmeli.
Nywele zako ni kama zulia la urujuani;
mfalme ametekwa na mashungi yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.