Wimbo 5:8
Song of Songs 5:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza: kama mkimpata mpenzi wangu, mtamwambia nini? Mwambieni ninazimia kwa mapenzi.
Song of Songs 5:8 in English
Song of Songs 5:8 · Berean Standard Bible
O daughters of Jerusalem, I adjure you, if you find my beloved, tell him I am sick with love.
Context
6Nilimfungulia mpenzi wangu,
lakini mpenzi wangu alishaondoka;
alikuwa amekwenda zake.
Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake.
Nilimtafuta lakini sikumpata.
Nilimwita lakini hakunijibu. 7Walinzi walinikuta
walipokuwa wakifanya zamu za ulinzi mjini.
Walinipiga, wakanijeruhi,
wakaninyangʼanya joho langu,
hao walinzi wa kuta! 8Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza:
kama mkimpata mpenzi wangu,
mtamwambia nini?
Mwambieni ninazimia kwa mapenzi. 9Je, mpendwa wako ni bora kuliko wengine namna gani,
wewe uliye mzuri kupita wanawake wote?
Je, mpendwa wako ni mzuri kuliko wengine, namna gani,
hata unatuagiza hivyo? 10Mpenzi wangu anangʼaa, tena ni mwekundu,
wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.