Wimbo 5:4
Song of Songs 5:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mpenzi wangu aliweka mkono wake kwenye tundu la komeo; moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili yake.
Song of Songs 5:4 in English
Song of Songs 5:4 · Berean Standard Bible
My beloved put his hand to the latch; my heart pounded for him.
Context
2(1) Kuleni, enyi marafiki, mnywe;
kunyweni ya kutosha, ee wapenzi. 3(2) Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho.
Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha:
“Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu,
hua wangu, asiye na hitilafu.
Kichwa changu kimeloa umande,
na nywele zangu manyunyu ya usiku.”
(3) Nimevua joho langu:
je, ni lazima nivae tena?
Nimenawa miguu yangu:
je, ni lazima niichafue tena? 4Mpenzi wangu aliweka mkono wake kwenye tundu la komeo;
moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili yake. 5Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu,
mikono yangu ikidondosha manemane,
vidole vyangu vikitiririka manemane,
penye vipini vya komeo. 6Nilimfungulia mpenzi wangu,
lakini mpenzi wangu alishaondoka;
alikuwa amekwenda zake.
Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake.
Nilimtafuta lakini sikumpata.
Nilimwita lakini hakunijibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.