Wimbo 5:11
Song of Songs 5:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote, nywele zake ni za mawimbi na ni nyeusi kama kunguru.
Song of Songs 5:11 in English
Song of Songs 5:11 · Berean Standard Bible
His head is purest gold; his hair is wavy and black as a raven.
Context
9Je, mpendwa wako ni bora kuliko wengine namna gani,
wewe uliye mzuri kupita wanawake wote?
Je, mpendwa wako ni mzuri kuliko wengine, namna gani,
hata unatuagiza hivyo? 10Mpenzi wangu anangʼaa, tena ni mwekundu,
wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu. 11Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote,
nywele zake ni za mawimbi
na ni nyeusi kama kunguru. 12Macho yake ni kama ya hua
kandokando ya vijito vya maji,
aliyeogeshwa kwenye maziwa,
yaliyopangwa kama vito vya thamani. 13Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo
yakitoa manukato.
Midomo yake ni kama yungiyungi
inayodondosha manemane.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.