Warumi 9:25
Romans 9:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama vile Mungu asemavyo katika Hosea: “Nitawaita ‘watu wangu’ wale ambao si watu wangu; nami nitamwita ‘mpenzi wangu’ yeye ambaye si mpenzi wangu,”
Romans 9:25 in English
Romans 9:25 · Berean Standard Bible
As He says in Hosea: “I will call them ‘My People’ who are not My people, and I will call her ‘My Beloved’ who is not My beloved,”*
Context
23Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vile vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake, 24yaani pamoja na sisi, ambao pia alituita, si kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa? 25Kama vile Mungu asemavyo katika Hosea:
“Nitawaita ‘watu wangu’
wale ambao si watu wangu;
nami nitamwita ‘mpenzi wangu’
yeye ambaye si mpenzi wangu,” 26tena,
“Itakuwa hasa mahali pale walipoambiwa,
‘Ninyi si watu wangu,’
wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ ” 27Isaya anapiga kelele kuhusu Israeli:
“Ingawa idadi ya wana wa Israeli
ni wengi kama mchanga wa pwani,
ni mabaki yao tu watakaookolewa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.