Native Bible

Romans 7:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu.

Romans 7:22 in English

Romans 7:22 · Berean Standard Bible

For in my inner being I delight in God’s law.

Context

20Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 21Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo. 22Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu. 23Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu. Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu. 24Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.