Warumi 6:20
Romans 6:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki.
Romans 6:20 in English
Romans 6:20 · Berean Standard Bible
For when you were slaves to sin, you were free of obligation to righteousness.
Context
18Nanyi, mkiisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mmekuwa watumwa wa haki. 19Ninasema kwa namna ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wenu wa hali ya asili. Kama vile mlivyokuwa mkivitoa viungo vya miili yenu kama watumwa wa mambo machafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi, hivyo sasa vitoeni viungo vyenu kama watumwa wa haki inayowaelekeza mpate kutakaswa. 20Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki. 21Lakini mlipata faida gani kwa mambo hayo ambayo sasa mnayaonea aibu? Mwisho wa mambo hayo ni mauti. 22Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakatifu, ambao mwisho wake ni uzima wa milele.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.