Warumi 6:18
Romans 6:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nanyi, mkiisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mmekuwa watumwa wa haki.
Romans 6:18 in English
Romans 6:18 · Berean Standard Bible
You have been set free from sin and have become slaves to righteousness.
Context
16Je, hamjui kwamba mnapojitoa kwa mtu yeyote kama watumwa watiifu, ninyi ni watumwa wa yule mnayemtii, aidha watumwa wa dhambi, ambayo matokeo yake ni mauti, au watumwa wa utii ambao matokeo yake ni haki? 17Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmekuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliyopewa. 18Nanyi, mkiisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mmekuwa watumwa wa haki. 19Ninasema kwa namna ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wenu wa hali ya asili. Kama vile mlivyokuwa mkivitoa viungo vya miili yenu kama watumwa wa mambo machafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi, hivyo sasa vitoeni viungo vyenu kama watumwa wa haki inayowaelekeza mpate kutakaswa. 20Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.