Warumi 15:22
Romans 15:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hii ndiyo sababu nimezuiliwa mara nyingi nisiweze kuja kwenu.
Romans 15:22 in English
Romans 15:22 · Berean Standard Bible
That is why I have often been hindered from coming to you.
Context
20Hivyo ni nia yangu kuhubiri Habari Njema, si pale ambapo Kristo amekwisha kujulikana, ili nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine. 21Lakini kama ilivyoandikwa:
“Wale ambao hawajahubiriwa habari zake wataona,
nao wale ambao hawajazisikia watafahamu.” 22Hii ndiyo sababu nimezuiliwa mara nyingi nisiweze kuja kwenu. 23Lakini sasa kwa kuwa hakuna nafasi zaidi kwa ajili yangu katika sehemu hii, ninatamani kuja kwenu kama ambavyo nimekuwa na shauku kwa miaka mingi. 24Nimekusudia kufanya hivyo nitakapokuwa njiani kwenda Hispania. Natarajia kuwaona katika safari yangu na kusafirishwa nanyi mpaka huko, baada ya kufurahia ushirika wenu kwa kitambo kidogo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.