Warumi 14:11
Romans 14:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Kama vile niishivyo,’ asema Bwana, ‘kila goti litapigwa mbele zangu, na kila ulimi utakiri kwa Mungu.’ ”
Romans 14:11 in English
Romans 14:11 · Berean Standard Bible
It is written: “As surely as I live, says the Lord, every knee will bow before Me; every tongue will confess to God.”*
Context
9Kwani kwa sababu hii hasa, Kristo alikufa na akawa hai tena kusudi apate kuwa Bwana wa wote, yaani, waliokufa na walio hai. 10Basi kwa nini wewe wamhukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sote tutasimama mbele ya kiti cha Mungu cha hukumu. 11Kwa kuwa imeandikwa:
“ ‘Kama vile niishivyo,’ asema Bwana,
‘kila goti litapigwa mbele zangu,
na kila ulimi utakiri kwa Mungu.’ ” 12Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu. 13Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.