Warumi 14:12
Romans 14:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu.
Romans 14:12 in English
Romans 14:12 · Berean Standard Bible
So then, each of us will give an account of himself to God.
Context
10Basi kwa nini wewe wamhukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sote tutasimama mbele ya kiti cha Mungu cha hukumu. 11Kwa kuwa imeandikwa:
“ ‘Kama vile niishivyo,’ asema Bwana,
‘kila goti litapigwa mbele zangu,
na kila ulimi utakiri kwa Mungu.’ ” 12Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu. 13Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine. 14Ninajua tena nimehakikishiwa sana katika Bwana Yesu kwamba hakuna kitu chochote ambacho ni najisi kwa asili yake. Lakini kama mtu anakiona kitu kuwa ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.