Native Bible

Romans 12:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao.

Romans 12:15 in English

Romans 12:15 · Berean Standard Bible

Rejoice with those who rejoice; weep with those who weep.

Context

13Changieni katika mahitaji ya watakatifu, wakaribisheni wageni. 14Wabarikini wale wanaowatesa, barikini wala msilaani. 15Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao. 16Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu. 17Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.