Native Bible

Romans 11:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, Mungu alimjibuje? “Nimejibakizia watu elfu saba ambao hawajapiga magoti kumwabudu Baali.”

Romans 11:4 in English

Romans 11:4 · Berean Standard Bible

And what was the divine reply to him? “I have reserved for Myself seven thousand men who have not bowed the knee to Baal.”*

Context

2Mungu hajawakataa watu wake, ambao yeye aliwajua tangu mwanzo. Je, hamjui yale Maandiko yasemayo kuhusu Eliya, jinsi alivyomlalamikia Mungu kuhusu Israeli? 3Alisema, “Bwana, wamewaua manabii wako na kuzibomoa madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua?” 4Je, Mungu alimjibuje? “Nimejibakizia watu elfu saba ambao hawajapiga magoti kumwabudu Baali.” 5Vivyo hivyo pia, sasa wapo mabaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu. 6Lakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, si tena kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa kwa matendo, neema isingekuwa neema tena.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.