Native Bible

Romans 10:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao.

Romans 10:12 in English

Romans 10:12 · Berean Standard Bible

For there is no difference between Jew and Greek: The same Lord is Lord of all, and gives richly to all who call on Him,

Context

10Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu. 11Kama yasemavyo Maandiko, “Yeyote amwaminiye hataaibika kamwe.” 12Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. 13Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa.” 14Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.