Ufunuo 7:16
Revelation 7:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kamwe hawataona njaa wala kiu tena. Jua halitawapiga wala joto lolote liunguzalo.
Revelation 7:16 in English
Revelation 7:16 · Berean Standard Bible
‘Never again will they hunger, and never will they thirst; nor will the sun beat down upon them, nor any scorching heat.’*
Context
14Nikamjibu, “Bwana, wewe wajua.”
Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa. 15Kwa hiyo,
“Wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu
na kumtumikia usiku na mchana
katika hekalu lake;
naye aketiye katika kile kiti cha enzi
atatanda hema yake juu yao. 16Kamwe hawataona njaa
wala kiu tena.
Jua halitawapiga
wala joto lolote liunguzalo. 17Kwa maana Mwana-Kondoo
aliyeko katikati ya kile kiti cha enzi
atakuwa Mchungaji wao;
naye atawaongoza kwenda
kwenye chemchemi za maji yaliyo hai.
Naye Mungu atafuta kila chozi
kutoka macho yao.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.