Ufunuo 2:26
Revelation 2:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Atakayeshinda na kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa:
Revelation 2:26 in English
Revelation 2:26 · Berean Standard Bible
And to the one who overcomes and continues in My work until the end, I will give authority over the nations.
Context
24Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo yanayoitwa mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wowote juu yenu): 25Lakini shikeni sana mlicho nacho, mpaka nitakapokuja. 26“Atakayeshinda na kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa: 27“ ‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma,
atawavunja vipande vipande
kama chombo cha udongo’:
kama vile mimi nilivyopokea mamlaka kutoka kwa Baba yangu. 28Nami nitampa pia ile nyota ya asubuhi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.