Ufunuo 13:9
Revelation 13:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye aliye na sikio na asikie.
Revelation 13:9 in English
Revelation 13:9 · Berean Standard Bible
He who has an ear, let him hear:
Context
7Pia akaruhusiwa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda. Akapewa uwezo juu ya watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa. 8Nao watu wote waishio duniani watamwabudu huyo mnyama, yaani, wale wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 9Yeye aliye na sikio na asikie. 10Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka,
atachukuliwa mateka.
Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga,
atauawa kwa upanga.
Hapa ndipo penye wito wa subira na imani ya watakatifu. 11Kisha nikamwona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka dunia. Alikuwa na pembe mbili kama mwana-kondoo, lakini akanena kama joka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.