Ufunuo 13:11
Revelation 13:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha nikamwona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka dunia. Alikuwa na pembe mbili kama mwana-kondoo, lakini akanena kama joka.
Revelation 13:11 in English
Revelation 13:11 · Berean Standard Bible
Then I saw another beast rising out of the earth. This beast had two horns like a lamb, but spoke like a dragon.
Context
9Yeye aliye na sikio na asikie. 10Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka,
atachukuliwa mateka.
Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga,
atauawa kwa upanga.
Hapa ndipo penye wito wa subira na imani ya watakatifu. 11Kisha nikamwona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka dunia. Alikuwa na pembe mbili kama mwana-kondoo, lakini akanena kama joka. 12Akatumia mamlaka yote ya yule mnyama wa kwanza kwa niaba yake, naye akawafanya wote wakaao duniani kumwabudu yule mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. 13Naye akafanya ishara kuu na za ajabu, hata kusababisha moto kushuka toka mbinguni kuja duniani watu wakiona waziwazi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.