Ufunuo 12:8
Revelation 12:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini joka na malaika zake wakashindwa, na hapakuwa tena na nafasi yao huko mbinguni.
Revelation 12:8 in English
Revelation 12:8 · Berean Standard Bible
But the dragon was not strong enough, and no longer was any place found in heaven for him and his angels.
Context
6Yule mwanamke akakimbilia jangwani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali ili apate kutunzwa huko kwa muda wa siku 1,260. 7Basi palikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na hilo joka, nalo joka pamoja na malaika zake likapigana nao. 8Lakini joka na malaika zake wakashindwa, na hapakuwa tena na nafasi yao huko mbinguni. 9Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwengu wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake. 10Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema:
“Sasa wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja
na mamlaka ya Kristo wake.
Kwa kuwa ametupwa chini
mshtaki wa ndugu zetu,
anayewashtaki mbele za Mungu
usiku na mchana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.