Ufunuo 11:9
Revelation 11:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe.
Revelation 11:9 in English
Revelation 11:9 · Berean Standard Bible
For three and a half days all peoples and tribes and tongues and nations will view their bodies and will not permit them to be laid in a tomb.
Context
7Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua. 8Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa,* ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri,* ambapo pia Bwana wao alisulubiwa. 9Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe. 10Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani. 11Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingia, nao wakasimama kwa miguu yao na wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.