Native Bible

Revelation 11:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani.

Revelation 11:10 in English

Revelation 11:10 · Berean Standard Bible

And those who dwell on the earth will gloat over them, and will celebrate and send one another gifts, because these two prophets had tormented them.

Context

8Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa,* ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri,* ambapo pia Bwana wao alisulubiwa. 9Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe. 10Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani. 11Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingia, nao wakasimama kwa miguu yao na wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu. 12Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njooni huku juu!” Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakiwa wanawatazama.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.