Ufunuo 11:8
Revelation 11:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa,* ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri,* ambapo pia Bwana wao alisulubiwa.
Revelation 11:8 in English
Revelation 11:8 · Berean Standard Bible
Their bodies will lie in the street of the great city—figuratively called Sodom and Egypt—where their Lord was also crucified.
Context
6Watu hawa wanao uwezo wa kufunga anga ili mvua isinyeshe wakati wote watakapokuwa wanatoa unabii wao. Nao watakuwa na uwezo wa kuyabadili maji kuwa damu na kuipiga dunia kwa kila aina ya mapigo mara kwa mara kama watakavyo. 7Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua. 8Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa,* ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri,* ambapo pia Bwana wao alisulubiwa. 9Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe. 10Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.