Zaburi 93
Psalms 93 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
1Bwana anatawala, amejivika utukufu;
Bwana amejivika utukufu
tena amejivika nguvu.
Dunia imewekwa imara,
haitaondoshwa. 2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;
wewe umekuwako tangu milele. 3Bahari zimeinua, Ee Bwana,
bahari zimeinua sauti zake;
bahari zimeinua sauti za mawimbi yake. 4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
Bwana aishiye juu sana ni mkuu. 5Ee Bwana, sheria zako ni imara;
utakatifu umepamba nyumba yako
pasipo mwisho.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.